Dole la kati lamponza Mchezaji Hashim Mussa wa Mwadui

bongoleo.com


Image result for tff
Mahala popote Nidhamu ni salaha kubwa na ni kitu muhimu sana lakini baadhi ya vijana na hata wazee wakati mwingine huchukulia poa bila kujali matokeo yake.


Wengi wetu tumezoea kunyosha dole la kati huku uswahili kwetu ni kawaida sana, mimi sijui maana yake lakini tafsi ya dole hiyo huwa ni tusi na sehemu ambazo zinahitaji nidhamu huwezi kunyosha dole lako hilo.

Dole linaponza bana, Mchezaji wa Mwadui Hashim Yahya Mussa amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kwa kosa la kuwaonyeshea kidole cha kati watazamaji kama ishara ya matusi baada ya filimbi ya kumaliza mchezo ilipopigwa.

Kitendo hicho kilifanyika katika mchezo uliochezwa Februari 8, 2020 katika uwanja wa Namfua mjini Singida.

Hata hivyo sharia kwa mchezaji anayefanya kitendo hicho ni kali na huenda mchezaji huo akafungiwa hata mechi tano au zaidi.

#1 Downloaded Personalized News App

Read in App for better experience

cancel confirm